Omba
Bonyeza hapa Kuomba EFTA sasa, vinginevyo endelea kusoma kupata sababu kubwa zaidi za kuwasiliana na EFTA na

Dhamana haihitajiki
Tofauti na benki nyingine nyingi Tanzania, EFTA haikutaki utoe dhamana ya aina yoyote ili ukopeshwe mashine.
Benki nyingine watakuuliza mali kama nyumba au magari kama dhamana kwa ajili ya mkopo wao. Hili ni kwa sababu EFTA wanakupa mkopo kwa kukodisha, ikiwa na maana kwamba hizo zana zenyewe zinaweza kufanya kazi kama dhamana ya EFTA.
Manufaa ni kwamba bado unabakiwa na dhamana ambayo waweza kuitumia kama mtaji wa kufanyia kazi na kuombea mkopo kukuza biashara yako.
Pia ina maana hauhitaji kupoteza muda na nguvu zako kupata hati za nyumba jambo ambalo huweza kuwa gumu na kuchukua muda mrefu.

Kipindi kirefu cha kulipa mara nyingine
Pale EFTA, tunaelewa kwamba mtaji wa kufanyia kazi waweze kuwa umebana mwanzoni mwa uwekezaji. Kama mteja, unapewa kipindi cha miezi miwili cha msamaha/neema unapopokea mashine zako kuanzisha shughuli zako na kupokea malipo toka kwa wateja. Ni baada tu ya siku sitini ndipo EFTA watataka rejesho la kwanza.
Baada ya hapa, kipindi cha miezi 36 kina maana kwamba marejesho yanagawanywa kwenye mafungu madogo madogo, jambo ambalo litaifanya biashara yako ipanuke. Katika benki nyingi, ungetakiwa kurejesha kabla hata mradi haujaanza kuleta faida. Kwa EFTA, unakuwa na fursa nzuri kabisa ya kupata mafanikio katika biashara yako.

Viwango vya chini vya riba
Kwa viwango shindani vya riba, EFTA wanatoa huduma mbadala wa benki zingine za kibiashara. Hata hivyo ukizingatia kwamba huhitaji kulipa kitu chochote hadi vifaa vyao vianze kazi, utakuta kwamba bidhaa za EFTA zinatoa thamani kubwa zaidi ya fedha. Kwa benki nyingi, unaanza kurejesha mkopo wako pale tu unapoondoka hapo benki.

Hapahitajiki mahesabu yaliyokaguliwa na mipango ya biashara.
EFTA, tunatambua kwamba kutayarisha mahesabu yaliyokaguliwa na pia mipango ya biashara vinaweza kuwa ghali na vyenye kuchukua muda kwa mjasiriamali.
Hata hivyo pia ni muhimu tuweze kuelewa biashara yako inafanyaje kazi. Hii ndiyo sababu, Wakati wa awamu ya maombi ya mkopo, EFTA watahitaji kuchanganua mzunguko wa fedha na faida katika biashara yako.
Mara nyingi hili huhitaji kuchunguza kwa kina kumbukumbu za mauzo yako, pamoja na kutembelea eneo lako la kazi ambapo tutakagua mazingira, kukutana na wateja na wafanyakazi wako. Wakati ambapo mahesabu yaliyokaguliwa yanakaribishwa, tunatafuta njia nyingine za kuweza kuijua biashara yako.

Uwazi
Tofauti na baadhi ya benki, hakuna malipo/ada mengine yaliyofichika kama vile malipo makubwa ya kuomba mkopo au malipo ya kushughulikia mkopo. EFTA, ni bure kuleta maombi na hutahitaji kufanya malipo yoyote hadi upokee barua ikikuambia umekubaliwa.