Ukurasa Wa BidHaa Zetu

Tunatoa mikopo ya mashine tu, zenye thamani ya kuanzia Shilingi milioni 20 na kuendelea. Kwa kuzingatia vigezo, tunaweza kutoa mikopo mikubwa zaidi kwa wateja wa kilimo biashara, au kwa wakulima wenye rekodi nzuri za kuaminika. Tuna bidhaa za aina nne:

 • Kawaida
 • Mashine Zinazojongea
 • Kurudia
 • Kuingiza
 • EFTA Huduma ya afya
 • Udhamini Wa Wasambazaji

Huduma ya mikopo ya EFTA ya kawaida inajumuisha malipo ya awali ya 10% hadi 30%, pamoja na kipindi cha miezi 36 cha marejesho kuanzia siku sitini baada ya kukabidhiwa.

Mashine zinazojongea za EFTA ni kwa vifaa vyote vinavyohamishika. Zinahitaji malipo ya wali ya asilimia ishirini 20%, na miezi 36 ya marejesho kuanzia siku sitini baada ya kukabidhiwa.

Bidhaa za EFTA za marudio ni kwa ajili ya wateja ambao awali wamekamilisha mkopo wa EFTA. Kama ilivyo kwa huduma ya mikopo ya kawaida, Bidhaa ya marudio inahitaji malipo ya awali ya asilimia 10%, na miezi 36 ya marejesho kuanzia siku sitini baada ya kukabidhiwa. Wakopaji wa marudio walio na kumbukumbu nzuri sana wanaweza kupatiwa fedha za ziada kwa masharti nafuu kuliko bidhaa ya kawaida.

Kwa wateja wanaotaka kuagiza mashine kutoka India, Kenya au China EFTA huhitaji asilimia 20 kama malipo ya awali ambazo EFTA huingia kwenye kuwathibitisha wasambazaji wa mashine hizo pamoja nakujiridhisha kuhusu ubora kabla ya mashine hizo kusafirishwa. EFTA huagiza kutoka nje ya Africa mashine zenye thamani ya milioni 60 au zaidi tu.

Wateja waliojiorodhesha au wanaohitaji kujiorodhesha kwenye huduma za afya salama EFTA wanaweza kuwakopesha vifaa kwa gaharama zenye riba ndogo kuliko huduma za kawaida. Gharama hizo zitajumuisha pia matengenezo ya hizo mashine katika kipindi cha miaka mitatu cha mkopo.

EFTA wana vigezo maalumu kupitia wauzaji waliopendekezwa. Kwa sasa EFTA wanaweza kutoa riba ndogo kwa wateja wanaokopa kupitia John Deere, ikiwamo na mwaka moja wa matengenezo bila malipo.

Unastahili kuomba mkopo?

Kustahili mkopo wa EFTA lazima uwe na:

 • Uwe anapatikana ofisi za EFTA zilipo.
 • Awe na uzoefu katika Biashara aliyombea mashine.
 • Hii biashara iwe ndio shughuli yako kuu.
 • Hatuwekezi kwenye usindikaji wa tumbaku au vileo.

Tunawafikiria pia wale wanaonza ili mradi waweze kuonyesha kuwa wanauzoefu wa kutoshana uwezo wa kutosha kuendesha biashara pamoja na wateja waliotarajiwa kununua badhaa zao au kutumia huduma watakazo zitoa.

Si lazima kuwa na kampuni iliyoandikishwa kisheria, kuwa na mahesabu yaliyokaguliwa au kuwa na historia yakuhifadhi fedha benki. Hata hivyo tutahitaji kuangalia vitabu vyako vya mauzo au kuongea na baadhi ya wateja wako au kufanya utaratibu unaofanana na huo kuweza kupima kiwango cha biashara yako.

Nini kinatokea pale mkopo wakoukipitishwa na EFTA.

Mkopo wako ukipitishwa utahitajika kuandaa leseni na vibali muhimu kwa ajili ya biashara yako kutoka kwa mamlaka husika. Pia utahitajika kuwa na vitu vingine muhimu kama umeme, maji kulingana na uhitaji wa biashara yako.

Inachukua muda gani mkopo wangu kupitishwa?

Baada ya maombi yako kufika EFTA utapigiwa simu na kuulizwa maswali rahisi. Na ikionekana kama EFTA wataweza kukukopesha utaalikwa kwenye semina, na pale kwenye semina utapewa fomu ya maombi ya mkopo. Baada ya kurejesha fomu yako utaratibu wa kukutembelea utapangwa na kufanyika. Kisha maofisa mikopo wetu watawasilisha maombi  ya mkopo kwenye idara husika kuomba mkopo upitishwe. Zoezi hili huchukua takribani mwezi mmoja tuu hivyo tungependa urudishe fomu yako ya maombi mapema.

Lini nitamiliki hizo mashine?

Utamiliki hizo mashine baada ya kipindi cha miaka mitatu, hii ndio sababu yakufanya wewe iwe muhimu kwako kuchagua mashine ambazo zinadumu kwa muda mrefu ili uendelee kupata faida zake hata baada ya kumaliza kurejesha mkopo wako.

EFTA wanjihusishaje kipindi hichi cha mkopo?

EFTA watakutembelea kuangalia unavyoenenda kila baada ya miezi mitatu kama malipo yatafanyika kwa wakati. Kama unahangaika namna ya kulipa EFTA watakutembelea kila mara na kukupa ushauri kibiashara, kufuatilia malipo endapo hayatafanika kwa wakati.

Kuna mafunzo yoyote yanyotolewa?

Kwa sasa EFTA wanatoa mafunzo ya afya na usalama mahali pa kazi, mafunzo ya utawala na rasimali watu. Hivi karibuni tutazindua mafunzo ya kuwahudumia wateja.

SMEs in developing countries

Caught in the Middle: EFTA's work in East Africa featured by the Economist

view article

News

 • 1 October 2016
  EFTA opens new branch in Dar es Salaam! The branch is located at IT Plaza on Ohio Street. Currently EFTA is only working with customers who work with an EFTA preferred supplier.
 • 8 August 2016
  Morogoro wins 3rd place for best Financial Institution for Farmers (after NMB and Finca); Mwanza wins 3rd best service provider among financial institutions at East African Exhibition (after CRDB and FNB)
 • 6 June 2016
  EFTA’s work with SMEs in Tanzania featured by the Economist.
 • 9 April 2016
  EFTA opens new branch in Morogoro, Tanzania on Madaraka Road – now able to serve the Morogoro region!
 • 9 December 2015
  EFTA opens new branch in Bukoba, Tanzania on Migeyo Street – now able to serve customers in Kagera!

EFTA Whistleblower hotline

Thank you for contacting the EFTA Whistleblower hotline. The purpose of this hotline is to allow EFTA’s customers, employees, suppliers and other stakeholders to share any observations regarding actions that you may feel or inappropriate or illegal, as well as any other actions that do not align with EFTA’s Code of Conduct. The information in the form below will be sent to an independent individual within the organization who will deal with the request swiftly and professionally.

Note that all concerns will be treated in confidence and every effort will be made not to reveal your identity, if that is your wish. If disciplinary or other proceedings follow the investigation, it may not be possible to take action as a result of your disclosure without your help, so you may be asked to come forward as a witness. If you agree to this, you will be offered advice and support.

Whistleblower

MAONI YAKO

Asante kwa kuwasiliana na EFTA. Kusudi la ukurasa huu ni kuruhusu wateja wa EFTA, wafanyakazi, wasambazaji na wadau wengine kushiriki katika kuripoti Kero yoyote kuhusu huduma au matendo yasiyofaa au yaliyo kinyume cha sheria, pamoja na vitendo vinginevyo visivyoendana na Kanuni na Maadili ya EFTA. 

Weka maelezo katika fomu hapa chini ambayo itatumwa kwa mtu binafsi/huru ndani ya shirika ambaye atashughulika na ombi au lalamiko lako.

Kumbuka taarifa zako zitahifadhiwa kwa siri na kila jitihada zitafanywa kutotoa utambulisho wako. Ikiwa msaada wako utahitajika ili kuruhusu uchunguzi wa kisheria, tutaomba ushirikiano wako na utapewa ushauri na usaidizi ili kulinda usalama wako.

Whistleblower Swahili

Menu Title