Akiwa anajitahidi kwenda na uhitaji huu, alirudi tena EFTA mwaka 2008 kununua mashine ya kutengeneza chakula cha kuku. Baada ya muda mfupi sana hii ikaja kuwa biashara yake kubwa, Mkopo wa mashine wa EFTA usio na sharti la dhamana ulimsaidia kupanua biashara yake kwa njia nyingine, amefanikiwa sana kiasi kwamba sasa ndiye msambazaji mkubwa wa chakula cha kuku Kaskazini mwa Tanzania.
Alipoulizwa ni kwa nini alichagua EFTA, ndugu Mushi alijibu kwamba EFTA ndiyo taasisi pekee ya kifedha inayotoa mikopo bila dhamana, kitu ambacho kingekuwa shida kwake kutimiza. Aliongeza kuwa wafanyakazi wa EFTA walikuwa tayari muda wote kutatua matatizo ya aina mbalimbali aliyokabiliwa nayo, jambo lililomrahisishia kufanya marejesho.
Ndugu Mushi sasa ameajiri watu 14.anapanga kuchukua mkopo mwingine wa zana kubwa zaidi toka EFTA ambayo itamsaidia chakula chenye umbo la vidonge, bidhaa ya hali ya juu zaidi kwenye soko la vyakula vya kuku.
“EFTA imenifanya niwe nilivyo leo, EFTA inawajali na kufanya ndoto za wajasiriamali kuwa kweli.” Anasema ndugu Mushi”